Uanachama

NAMNA YA KUWA MWANACHAMA WA THTU

Wafanyakazi wote wa SUA wana hiari ya kuwa wanachama wa THTU kama sheria za kazi zinavyolekeza juu ya uhuru wa wafanyakazi kujumuika pamoja kwa hiari.

Masharti ya kuwa mwanachama wa THTU

  1. Mwanachama wa THTU sharti awe mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na awe ni raia wa Tanzania.
  2. Ajaze fomu maalum ya kujiunga na chama cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria.
  3. Maombi ya wanachama wapya yatapelekwa kwenye ofisi ya katibu wa tawi mahala pa kazi anapofanyia kazi muombaji.
  4. Uongozi wa tawi, bila kuchelewa, utachambua, kufikiria na kuyakubali maombi hayo. Uongozi wa tawi ukiyakataa maombi, utawajibika kutoa sababu za uamuzi huo kwa halmashauri ya tawi.
  5. Tawi litawasilisha Fomu/Taarifa hizo Makao Makuu ya Chama.

MADHUMUNI YA CHAMA (THTU Goals)

  1. Kusimamia na kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi mahali pa kazi.
  2. Kushirikiana, kujadiliana na waajiri kudumisha amani kwa kuboresha mazingira na maslahi ya wafanyakazi mahali pa kazi.
  3. Kuhakikisha kwamba mwajiri anafuata na kuziheshimu sheria za kazi.
  4. Kulinda, kuheshimu, na kutekeleza makubaliano ya pamoja yaliyojadiliwa na kukubaliwa kati ya chama na mwajiri.
  5. Kutekeleza na kusaidia katika utekelezaji wa mikataba ya hali bora za kazi, tuzo na kanuni za nidhamu kulingana na sheria za kazi.