Kuhusu THTU

MAANA YA CHAMA CHA WAFANYAKAZI

Chama cha wafanyakazi ni Chama cha hiari na kidemokrasia ambacho kinaundwa na wafanyakazi kwa madhumuni ya kulinda  na kudumisha maslahi yao ya pamoja na kuboresha hali zao za maisha.

Kifungu cha Nne (4) cha sharia ya Ajira na mahusiano Kazini, 2014 kuhusu tafsiri kinaeleza kwamba “Chama cha Wafanyakazi’’ maana yake ni idadi yoyote ya wafanyakazi walioungana pamoja kwa lengo, ikiwa kwa lengo hilo tu au kwa malengo mengine, la kuratibu mahusiano kati ya wafanyakazi na waajiriwa wao au Chama cha waajiri ambako waajiri wamejiunga.

Kazi (Functions) za Chama cha wafanyakazi ( Trade union Representatives) zimeainishwa katiak Kifungu cha 62(40 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, 2004.

KAZI ZA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI MAHALI PA KAZI

Viongozi wa chama cha wafanyakazi kwa ujumla wao hufanya kazi ambazo ni za Chama cha wafanyakazi kw mujibu wa Katiba ya Chama ama kwa mujibu wa Sheria. Katika kulinda na kudumisha maslahi ya wafanyakazi na kufikia malengo yake Chama cha Wafayakazi kupitia niongozi wake hufanya kazi nyingi mahali pa kazi katika ngazi mbalimballi kam ifuatavyo;

  1. Ulinzi: Viongozi wa chama cha wafanyakazi wanatakiwa kulinda wafanyakazi dhidi ya unyonyaji wa aina yoyote unao weza kufanywa na mwajiri. Viongozi wanatakiwa kulinda wafanyakazi dhidi ya
  • Uonevu
  • Unyanyasaji
  • Udhalilishaji
  • Ukandamizaji
  • Vitendo visivyokubalika (unfair labour practices) vinavyoweza kufanywa na mwajiri.
  1. Kuboresha hali za maisha: viongozi wanatakiwa kuhakikisha kuwa kwa kadri inavyowezekana hali za kimaisha za wafanyakazi zinaboreshwa kwa kusimamia upatikanaji wa mishahara inayoendana na hali ya maisha (fair wages), mazingira mazuri ya kufanyia kazi, huduma za kiustawi, kiusalama na kiafya kwa wafanyakazi.
  • Kushughurikia manung’uniko: viongozi wanatakiwa kusaidia wafanyakazi katika kuhakikisha kuwa manug’uniko(grievances) yao yanashughulikiwa mapema, na haraka kabla hayajafikia hatuia mbaya na kuzaa migogoro ya kikazi(labour disputes).
  1. Kushiriki katika majadiliano ya pamoja; kwa sehemu kubwa kamati ya majadiliano kwa upande wa wawakilishi wa wafanya kazi huundwa na viondozi wa chama cha wafanyakazi. Kwaiyo viongozi wanao wajibu wa kushiriki kikamilifu kwa kutumia mbinu za majadiliano (negotiation skills) katika kujadili masuala mbalimbali ya kiajira yanayoletwa kwenye meza ya majadiliano kwa lengo la kufikia makubaliano.
  2. Ushirikishwaji (participation) : viongozi wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika mijadala ndani ya baraza la wafanyakazi ili kuhakikisha kwamba maslahi ya wafanyakazi yanazingatiwa na kutetewa.
  3. Uelimishaji: viongozi wa chama cha wafanyakazi wanao wajibu wa kuelimisha wafanyakazi kuhusiana na mambo mbalimbali ya kiajira kwa kuendesha mafunzo ya elimu kazi kwa wafanyakazi kupitia mikutano, warsha, na semina, mahali pa kazi.
  • Ustawi na burudani: viongozi wano wajibu kuhakikisha kuwa sehemu ya kazi inakuwa ni sehemu inayovutia si kwa wafanyakazi kufanya kazi tu lakini pia wafanyakazi kuweza kupata huduma za kiustawi na burudani. Kuhakikisha kuwa huduma mbalimbali za kiustawi na burudani kama vile michezo huduma za chakula , huduma za maktaba n.k.
  • Uwakilishi : viongozi wanatakiwa kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanapatiwa uwakilishi wa kutosha katika mambo mbalimbali yanayowasibu mahali pa kazi kwa mujibu wa katiba na Saheria. Viongozi wanatakiwa kuwawakilisha wafanyakazi katika kushughulikia masuala yafuatayo;
  • Manung’uniko
  • Masuala ya kinidhamu
  • Migogogro ya kikazi

Vile vile viongozi wanatakiwa kuwawakilisha wafanyakazi katika shughulikia masuala mbalimbali katika vyombo vifuatavyo.

  • Kamati ya majadiliano ya pamoja
  • Baraza la wafanyakazi
  • Kamati ya nidhamu
  • Kamisheni ua usuluhishi na uamuzi (CMA)

 

WAJIBU/MAJUKUMU YA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI

Kama vile kiongozi wa chama cha wafanyakazi alivyo na haki zake, pia kwa upande mwingine ana wajibu au majukumu yanayokwenda sambamba na haki hizo. Yafuatayo ni daadhi ya majukumu yake;

  • Kutoa huduma kwa wanachama(service provider)
  • Kutetea wanachama anapofikwa na matatizo ya kikazi(advocacy and problem solver)
  • Kuwawakilisha wanachama katika vyombo mbaimbali (representative).
  • Kushiriki katika shughuri zote za chama na mikutano kwa mujibu wa katiba na sharia (active participant).
  • Kuwa tayari kutoa majibu ya masuala yoyote yenye utata kwa wanachama yahusuyo chama.
  • Kufanya maandalizi ya kushiriki kwenye shughuli za chama
  • Kuunga mukono na kusaisaidia kwa videndo maendeleo ya chama, taasisi na Taifa kwa ujumla.
  • Kuzingatia katiba, kanuni za chama na sharia za nchi na kuheshimu na kutekeleza kwa vitendo maamuzi yatokanayo na vikao.
  • Kulinda, kutetea na kutekeleza katiba ya chama.
  • Kutoa elimu kwa wanachama